Mogela ana neno kwa wachezaji Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
9 Jan 2018
Mogela ana neno kwa wachezaji Simba
Simba imeshatolewa kwenye michuano ya Kombe la FA na kusaliwa na tiketi moja ya ushiriki wa michuano ya kimataifa mwakani, yaani kupitia Ligi Kuu Bara kama itatwaa ubingwa na sasa nyota wa zamani wa klabu hiyo, Zamoyoni Mogella, amewashtua wachezaji wa timu hiyo.

Mogella amesema nyota wa Simba kama hawatakaza ligi itakapoendelea, basi wajue wazi watabeba lawama, hivyo lazima wajipange kweli kweli kuhakikisha timu yao haishuki katika msimamo wa ligi hiyo.

Simba ambayo jioni ya jana ilitolewa pia katika Kombe la Mapinduzi baada ya kulala bao 1-0 mbele ya URA, inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa sasa ikiwa na alama 26 sawa na Azam ila ikiwa na faida ya mabao ya kufunga.

“Ikumbukwe FA ndilo iliyowapa nafasi Simba kushiriki michuano ya kimataifa mwaka huu, sasa walishatolewa, wameenda Zanzibar nako wameyumba, ni vema wakajipanga kwa mechi za Ligi Kuu ili kuwapa raha mashabiki wao,” alisema Mogella.

Naye winga wa zamani wa timu hiyo, Ulimboka Mwakingwe, amewataka wachezaji wa Simba kuangalia mbali katika soka la klabu yao na maisha yao.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
48m ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →