Simba kujichimbia kambini kuiwinda Mwadui Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Jan 2020
Simba kujichimbia kambini kuiwinda Mwadui Fc

Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo kinaingia kambini kujiandaa na mchezo wa raundi ya nne kombe la Azam (ASFC) dhidi ya Mwadui Fc

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema timu itaweka kambi ndege Beach nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam

Rweyemamu amesema wachezaji wote waliosajiliwa na Simba wataingia kambini kujiandaa na mchezo huo ambao utapigwa Jumamosi Januari 25 katika uwanja wa Uhuru

"Leo timu itaingia kambini Ndege Beach tulipoweka kambi ya kudumu katika msimu huu kujiandaa na mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Mwadui," ameesema

"Tunafahamu umuhimu mkubwa wa kombe hili, hivyo ni lazima timu yetu ipate matokeo mazuri ili tuendelee na mashindano hayo na mwisho wa siku tuweze kuwa mabingwa"

"Maandalizi yanakwenda vizuri na timu yetu  na wachezaji wote wataingia kambini akiwemo kiungo Shiza Kichuya ambaye alikuwa akikamilisha baadhi ya mambo ili aanze kuichezea Simba"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
3h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
3h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
6h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’