Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amewasifu wachezaji wa timu hiyo kuwa wamekuwa wepesi wa kuelewa kile anachowaelekeza
Akizungumza baada ya kurejea kutoka jijini Mwanza alikoiongoza timu yake kupata ushindi dhidi ya Mbao Fc na Alliance Fc, Vandenbroeck amesema siri ya mafanikio wanayopata ni juhudi za wachezaji lakini pia kutekeleza kwa ufasaha kile wanachoelekezwa
Mbelgiji huyo amejinasibu kuwa timu yake imekuwa ikitumia mfumo wa 4-3-3 ni mfumo huo unaowapa mafanikio
βMfumo wangu ni 4-3-3 ambao ndiyo nautumia kila mechi, mara zote nacheza kwa mfumo huo na ndiyo umetupa ushindi hadi sasa," alisema Vandenbroeck
"Tukicheza hivyo tunakuwa na kasi sana na tunacheza kwa haraka zaidi ya wengine, jambo ambalo ndiyo linatufanya hadi sasa kushinda mechi zetu hizi ambazo nimesimama hadi sasa"
Vandenbroeck ameisimamia Simba katika michezo sita, ameshinda michezo mitano na kutoka sare mmoja tu dhidi ya Yanga
Ameshinda michezo dhidi ya Lipuli FC mabao 4-0, KMC 2-0, Ndanda 2-0, Mbao FC 2-1 na Alliance Fc mabao 4-1