Baada ya Simba kutolewa kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi, wadau wa soka wamekosoa mfumo uliotumiwa na Kaimu Kocha wa Simba Masudi DJuma kuwa ni chanzo cha timu hiyo kufanya vibaya.
Aidha wako wanao amini kuwa Simba ilifanya makosa kumuondoa aliyekuwa kocha wake Joseph Omog kwani tatizo la Simba halikuwa kocha.
Wanaokosoa mfumo wanazo sababu za msingi kwani Simba haikuwahi kutumia mfumo wa walinzi watatu nyuma, ni dhahiri wachezaji watahitaji muda kuuelewa mfumo huo.
Pengine Djuma angefaa aendelee na mfumo aliokuwa akiutumia Omog kwa kuwa ndio wachezaji wanaufahamu zaidi huku akiendelea kuwafundisha mfumo wake taratibu na pengine angeutumia mfumo huo kwenye baadhi ya michezo tu.
Pia kitaalamu wanasema kuna mifumo inahitaji wachezaji wa aina yake ili uweze kuitumia. Simba hii ilitengenezwa wakati wa Omog ambaye hakuwa akitumia wachezaji watatu nyuma.
Matokeo yake tumeshuhudia wachezaji wa pembeni waliokuwa wakitumika kwa nyakati tofauti Gyan, Kichuya, Kwasi na Kotei wakijisahau kurejea kuzuia mashambulizi hivyo kutoa mwanya kwa wapinzani kutumia nafasi zao kufunga mabao.
Mabao iliyofungwa Simba na Azam FC, URA yamesababishwa na uwepo wa mwanya pembeni baada ya walinzi/washambuliaji wa pembeni kuchelewa kurudi kuzuia.
Lakini ni mfumo mzuri kama wachezaji wataweza kuuelewa.
Swala la wachezaji kujituma linaelezwa kuwa sababu nyingine inayoikwamisha Simba katika siku za hivi karibuni.
Kumekuwa na utofauti mkubwa kati Simba iliyoanza msimu na hii ya sasa. Ile kasi ya wachezaji imeonekana kupotea. Wachezaji wamekuwa wakicheza taratibu, bila presha kama wameshinda mabao mengi.
Baadhi ya wachezaji vinara kama Shiza Kichuya wanaonekana kushuka viwango kadiri siku zinavyokwenda, pengine ni uchovu wa kucheza michezo mingi mfululizo, wanahitaji kupumzishwa kwenye baadhi ya michezo.
Ni sahihi kwa mashabiki wa Simba kupaza sauti zao kwani kwa kiwango hiki kilichoonyeshwa kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi, ni ndoto kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom.
Ni muhimu kwa benchi la ufundi kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye michuano hiyo kwa haraka kabla michezo ya ligi kuu ya Vodacom haijarejea baada ya kukamilika kwa michuano ya kombe la Mapinduzi.

ADVERTISE HERE