Baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Alliance Fc jana, kikosi cha Simba kimeondoka jijini Mwanza kurejea Dar tayari kwa mchezo unaofuata
Mabingwa hao wa nchi wamekamilisha vyema ratiba yao ya jijini Mwanza wakishinda mechi zote mbili
Kabla ya mchezo wa jana, waliichapa Mbao Fc mabao 2-1
Alhamisi Januari 23 watashuka katika uwanja wa Uhuru kuikaribisha Mwadui Fc katika mchezo wa kombe la Azam duru ya nne
ADVERTISE HERE