Happy BirthDay Haji Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Jan 2020
Happy BirthDay Haji Manara

Saa 4 usiku wa Jumamosi ya January 18, Katikati ya jiji la Dar, Bint mrembo na mng'avu,mtoto wa Mzee Hassan Haji aitwae Bi Rahma anajifungua mtoto mzuri na mwenye afya.

Nakuzungumzia wewe Haji Sunday Ramadhan Manara "De la Boss" mtoto wa nyota wa kwanza Tanzania aliyeanza kucheza soka Ulaya na Asia katika vilabu vya Heracles, New York Eagles, Australian Club na Al Nasri. *Happy Birthday to you Soldier!!!* Tabia ya udadisi,usikilizaji hoja na kupenda kujudge mambo vimekuwa sehemu tu ya kichocheo cha mafanikio yako.

Yes!!, umeweza kuongeza mtaji wa rasilimali watu toka pale kaka Steven Ally alipoutangazia umma wa wana Simba na wanamichezo kwa ujumla kuwa utachukua nafasi ya Kaka Humphrey Nyansio.

Hapo kabla Simba haikuizidi Yanga kwa mashabiki lakini leo wazi kabisa na hili nakiri mie kama mzoefu wa soka hapa nchini,wazi kabisa Simba ina washabiki wengi ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa sehemu ya maendeleo makubwa ya klabu.Pamoja na hayo umefanya hamasa kurejea upya vinapokutana vilabu hivi viwili vya watani wa jadi (Traditional rivals). Wana Simba hatuwezi kusahau slogan kama "This is Simba"
"Yes We Can"
"Do or Die" nk

Naandika haya kama mdau mzoefu wa mpira, haijawahi kutokea hapa Tanzania haswa kwa klabu yetu akatokea mtu tena wa kawaida asiye na kipato kuweza kuhamasisha watu kwa namna hii.

Mwenyezi Mungu amwondoshe na adhabu ya kaburi wajina wako aliyekutabiria mema ya kuwa siku moja utakuwa mwenye jina kubwa na jasiri hapa Tanzania.

Wasiofahamu ni kuwa Mzee Hassan Haji (babu yako ) ni miongoni mwa wenyeviti waliowahi kuitumikia klabu yetu ya Simba miaka ya nyuma.

Makala hii imeandikwa na Al Hassan Mbilili, Mwanachama wa klabu ya Simba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’