Aussems awajibu mashabiki wanaotaka arudi Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Jan 2020
Aussems awajibu mashabiki wanaotaka arudi Simba

Aliyekuwa Mkufunzi wa Simba Patrick Aussems amesema amewasikia mashabiki wakishinikiza uongozi umrudishe lakini kwa upande wake hafikirii kurejea nchini Tanzania

Aussems alitimuliwa na Simba mwezi Novemba 2019 baada ya kutolewa mapema kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kuipa ubingwa timu hiyo na kucheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza

Kocha huyo ameanza kutajwa na mashabiki wa timu hiyo wakiutaka uongozi kumrejesha kwenye timu baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa, ambapo mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo Mo Dewji alitangaza kujiuzulu kabla ya kutangaza kurejea tena.

Aussems amesema kwa upande wake haoni jambo la kushangaza kwa yanayoendelea Simba lakini hakifirii kurejea kutokana na alichofanyiwa awali.

"Siyo jambo zuri kutaka kujua nini wanachokutana nacho Simba kwa sababu kwangu sioni kama kuna kitu kipya ambacho naweza kusema kwa kuwa wanavuna walichopanda wakati naondoka," alisema Aussems

"Unajua katika maisha unapata kile ambacho unastahili kupata na siyo unachotaka kupata sasa na wao wamepata wanachostahili, kifupi siwezi kurejea Simba kwa sababu ilishapita naangalia mambo yangu mengine"

Tangu aondoke Simba Aussems bado hajapata timu ingawa mwenyewe amesema ameamua kupumzika kwa muda kabla ya kurejea tena kwenye majukumu yake

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’