Kurudi Stars bado - Kapombe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Jan 2020
Kurudi Stars bado - Kapombe

Beki bora zaidi wa pembeni upande wa kulia kwa sasa hapa Tanzania Shomari Kapombe amesema bado anahitaji muda wa kujiimarisha kabla ya kufikiria kurudi timu ya Taifa

Kapombe jana aliiongoza Simba mkoani Mwanza kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao Fc katika mchezo uliopgwa uwanja wa CCM Kirumba

Beki huyo mwenye 'mapafu ya mbwa' kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusukuma mashambulizi mbele pamoja na kuzuia, alikuwa bora kwenye mchezo huo

Akizungumza baada ya mchezo, Kapombe alisema ushindi waliopata ni matokeo ya mbinu walizopewa na kocha Sven Vandenbroeck

"Tunamshukuru Mungu kwa kuweza kupata ushindi leo. Haukuwa mchezo rahisi lakini tuliweza kutumia nafasi tulizopata," alisema

Lakini pia waandishi walitaka kufahamu msimamo wake kama ikitokea ameitwa timu ya Taifa kutokana na ubora ambao ameendelea kuonyesha

"Kwa sasa bado siwezi kurudi timu ya Taifa kwani nahitaji kuimarika zaidi. Kikubwa tuendelee kumuomba Mungu labda kwa baadae naweza kurejea"

Kapombe alitangaza kustaafu kuchezea timu ya Taifa mwishoni mwa mwaka jana kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara

Mwaka juzi alivunjika mguu wakati akiitumikia Stars nchini Afrika Kusini jeraha ambalo nusura limalize maisha yake ya soka kwani alikaa nje kwa zaidi ya miezi nane

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’