Makonda atoa pole, haamini kama Mo amejiuzulu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Jan 2020
Makonda atoa pole, haamini kama Mo amejiuzulu

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda ambaye ni mdau mkubwa wa klabu ya Simba ametoa pole kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kupoteza mchezo wa fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi kwa kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar jana

Aidha kuhusu ujumbe wa Mo aliyetangaza kujiuzulu Uwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Makonda amesema haamini kama ujumbe huo umeandikwa na Mo mwenyewe

Amewataka Wanasimba kuwa watulivu kwani ukweli utafahamika

"Matokea ya Mpira huleta furaha na huzuni kwa wanaofungwa. Natoa pole Kwa team yangu ya Simba pamoja na Mashabiki wote na wanaoitakia mema SIMB," ameandika Makonda kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram

"Sina uhakika na kinachoendelea kwenye Akaunti ya MO kama ni @moodewji mwenyewe ameandika. Nawaomba wanasimba tutulie tutapata ukweli muda si mrefu. Tusisahau kuwa Wapo watu pia wabaya hutumia mwanya huu kuvuruga Amani na utulivu wa Team zetu. Simba nguvu moja"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’