Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ametangaza kujiuzulu Uwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi lakini ataendelea kubaki katika uwekezaji
Mo ametangaza uamuzi huo muda mfupi baada ya Simba kupoteza mchezo wa fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar
"Ni bahati mbaya Simba haikupata ushindi leo. Baada ya kulipa mishahaara inayofikia karibu Bilioni nne kwa mwaka, najiuzulu kuwa Mwenyekiti wa Bodi na kubaki kuwa Mwekezaji. Nitajikita katika kutengeneza miundombinu pamoja na Academy," sehemu ya ujumbe wa Mo imesomeka

ADVERTISE HERE