Rekodi zaibeba Simba fainali kombe la Mapinduzi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Jan 2020
Rekodi zaibeba Simba fainali kombe la Mapinduzi

Leo sio mara ya kwanza kwa Simba kukutana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa fainali michuano ya kombe la Mapinduzi

Mwaka 2015 Simba ilitwaa ubingwa wa Mapinduzi kwa ushindi wa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya matokeo ya sare

Mechi hiyo inayotarajiwa kupigwa kuanzia saa 2:15 usiku ni kama marudio ya fainali ya hiyo

Mtibwa Sugar imefika hatua hiyo baada ya kuitoa Chipukizi kwa mikwaju ya penalti 4-2 katika hatua ya mtoano kufuatia sare ya bao 1-1 na kisha nusu fainali kuitupa nje Yanga kwa idadi hiyo ya penalti kutokana na sare ya 1-1.

Simba yenyewe, hatua ya mtoano iliichapa Zimamoto mabao 3-1 kisha nusu fainali ikaitoa Azam FC kwa penalti 3-2 kufuatia dakika 90 kumalizika kwa sare tasa.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven amesema utakuwa mchezo mgumu kwa timu hizo zinazotoka Ligi Kuu Bara kukutana leo, lakini wamejiandaa vema na wanachotaka ni kombe la kwanza mwaka huu.

Amesema Mtibwa Sugar ni timu nzuri na inacheza soka la kuvutia, lakini hiyo haiwezi kuwa sababu kwao kukata tamaa.

"Mechi ya fainali hakuna timu ndogo na Mtibwa wanacheza vizuri, ila tunachotaka ni kombe," alisema.

Mbelgiji huyo alisema anashukuru katika mechi zilizopita hakukujitokeza majeruhi jambo ambalo linampa wigo mpana wa kupanga kikosi chake.

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Katwila, akiwa na kumbukumbu ya kulibeba kombe hilo wakati akiwa mchezaji wa timu hiyo mwaka 2010, alisema anafahamu Simba ni timu bora na wamejipanga kwa hilo.

Katwila alisema ukishafika fainali utarajie kukutana na timu bora, lakini si hilo tu anatambua ubora wa Simba mwaka huu hivyo itakuwa mechi ngumu.

"Tumekuja kupambana na tunataka kombe ingawa tunajua mechi itakuwa ngumu kwa kila upande," alisema kocha huyo ambaye mwaka 2010 akiwa mchezaji walilitwaa kombe hilo kwa kuifunga Ocean View katika mchezo wa fainali.

Bingwa wa michuano hiyo mbali na kombe na medali za dhahabu atajinyakulia Sh. milioni 15, huku mshindi wa pili akilamba Sh. milioni 10 na medali za fedha.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’