Hatutawadharau Mtibwa Sugar - Vandenbroeck

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Jan 2020
Hatutawadharau Mtibwa Sugar - Vandenbroeck

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema wanajipanga kikamilifu kuikabili Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa fainali michuano ya kombe la Mapinduzi

Mchezo huo utapigwa kesho Jumatatu, Januari 13 kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar

Simba ilitinga fainali ya michuano ya hiyo kwa kuiondosha Azam Fc kwa ushindi wa mikwaju ya penati 3-2 baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana

Wapinzani wao Mtibwa Sugar waliingia fainali kwa kuiondosha Yanga kwa penati 4-2 baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1

Vandenbroeck amesema wataingia katika mchezo huo bila ya kuwadharau wapinzani wao kwani anaamini hawakubahatisha kutinga fainali

Amesema wamedhamiria kutwaa taji la michuano hiyo ambayo hufanyika kila mwaka kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar

Naye kocha msaidizi Selemani Matola amesema ubora wa kikosi chao unawapa sababu ya kujiamini kuwa watapata ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar kesho

Simba imekuwa gumzo visiwani Zanzibar kutokana na aina ya soka lao ambalo linawapa burudani mashabiki wanaohudhuria michuano hiyo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’