Droo ya raundi ya nne michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ilifanyika juzi ambapo mabingwa wa Tanzania Bara Simba walipangwa kucheza na Mwadui Fc katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Uhuru kati ya Januari 24 na 26 2020
Huo utakuwa mchezo wa pili kuzikutanisha timu hizo msimu huu ambapo mchezo wa kwanza ambao ulikuwa wa ligi, Mwadui Fc iliichapa Simba bao 1-0
Kocha wa Mwadui Fc Khalid Adam amekiri mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa kikosi cha Simba na kubwa zaidi ni matokeo ya mchezo waioshinda kwenye ligi
Adam amesema anafahamu Simba itaingia kwenye mchezo huo kama nyati aliyejeruhiwa na hawatakubali kufungwa kwa mara ya pili
“Najua kabisa Simba hawatakubali tuwafunge kwa mara ya pili, lakini na sisi hatutakubali watufunge, tutacheza ugenini, kama kocha nitafanya maandalizi mazuri,” alisema Adam.
Tofauti na msimu uliopita, msimu huu Simba imeweka mkazo katika michuano yote inayoshirki
Katika mchezo wa raundi ya tatu kombe la Shirikisho waliifumua Arusha Fc mabao 6-0 kwenye mchezo ambao walitumia kikosi chao kamili
Sasa Simba iko visiwani Zanzibar ambako imetinga fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi ikitarajiwa kucheza na Mtibwa Sugar kesho
Simba inashiriki michuano hiyo ikitumia kikosi chake cha kwanza