Sven ataja sifa za beki anayemtaka Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Jan 2020
Sven ataja sifa za beki anayemtaka Simba

Dirisha dogo la usajili linaelekea ukingoni ambapo litafungwa Jumatano ijayo, Januari 15 2020 saa 5:59 usiku

Juzi Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa alikiri kupokea mapendekezo ya Sven ambapo wanahitaji kuyafanyia kazi kabla ya dirisha la usajili kufungwa

Inaelezwa Sven ametaka kusajiliwa wachezaji wawili ambao ni mlinzi wa kati na mshambuliaji

Lakini Mbelgiji huyo ametaka mlinzi ambaye atasajiliwa ni lazima awe anatumia mguu wa kushoto

Walinzi wote wa kati wa Simba wanatumia miguu ya kulia Erasto Nyoni pekee ndiye mwenye uwezo wa kutumia mguu wa kushoto ingawa sio asili yake

Sven amebainisha kuwa beki wa kati anayetumia mguu wa kushoto anakuwa na faida zaidi anapomkaba mshambuliaji anyetumia mguu wa kulia

 "Ni kweli nahitaji kufanya usajili wa beki mmoja wa kati kabla ya dirisha kufungwa. Nadhani ningependa zaidi kama angekuwa anatumia mguu wa kushoto kama yule wa Yanga (Ally sonso) kwakuwa inakuwa ni rahisi kumdhibiti mshambuliaji anayetumia mguu wa kulia," Sven alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

Misimu miwili iliyopita Simba ilikuwa na Salum Mbonde aliyemsajiliwa kutoka Mtibwa Sugar lakini aliachwa mwezi Julai baada ya mkataba wake kumalizika

Mbonde alikuwa majeruhi kwa muda mrefu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’