Pamoja na kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Azam Fc jana na baadae kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati, Simba iliupiga mpira mwingi sana
Ulikuwa mchezo ambao Simba ilitawala kila idara, vijana walicheza kwa kasi changamoto ikibaki kwenye matumizi ya nafasi walizotengeneza
Chini ya benchi jipya la ufundi linaloongozwa na Sven Vandenbroeck akisaidiwa na Selemani Matola, Simba imeendelea kuwa bora
Kwa mpira waliocheza Simba dhidi ya Azam jana, kama ingekuwa timu nyingine pengine wangeweza kuondoka na ushindi mnono
Azam Fc ni moja ya timu bora Tanzania kwa sasa
Pengine utagundua kwa nini Yanga walikubali kutolewa kirahisi na Mtibwa Sugar
Kwani kwa Simba hii sidhani kama wangeweza kupata hata sare kama walivyobahatisha kwenye mchezo wa ligi kuu wiki iliyopita
Β
Β