Mabingwa wa Tanzania Bara Simba wametinga fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi wakiibuka kwa ushindi wa mikwaju ya penat 3-2 baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana dhidi ya Azam Fc
Waliofunga mikwaju ya penati za Simba ni Erasto Nyoni, Jonas Mkude na John Bocco
Simba ilitawala dakika 90 za mchezo huo, ingeweza kuibuka na ushindi kwenye muda huo kama safu ya ushambuliaji ingetumia nafasi nyingi walizotengeneza
Mabingwa hao wa nchi sasa watachuana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa fainali ambao utapigwa Januari 13 2020
ADVERTISE HERE