Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mbatha, amethibitisha kupokea ripoti ya kocha Sven Vandenbroeck akisema muda wowote kuanzia sasa, wataanika kila kitu.
Senzo amesema wanaifanyia kazi kulingana na mapendekezo yake
Amesema kupitia ripoti hiyo, wameshafahamu ni maeneo gani ambayo yanahitaji maboresho na wachezaji ambao wanastahili kucheza hizo nafasi.
"Hatuwezi kuweka wazi kitu chochote kwa sasa kwani ni tupo kwenye mipango ya kuangalia ni jinsi gani tutafanikiwa kuyatimiza maelekezo yake," Senzo amenukuliwa na gazeti la Bingwa
Amesema baada ya kumnasa kiungo Luis Miquissone kutoka Mamelodi Sudown ya Afrika Kusini, kuna mchezaji mwingine atatua kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili Januari 15
ADVERTISE HERE