Kiungo mshambuliaji wa Simba Luis Miquissone ambaye alisajiliwa na mabingwa hao wa nchi wiki iliyopita, anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Azam Fc katika mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi leo
Miquissone alicheza kwa takribani dakika 13 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Zimamoto
Leo huenda akapewa dakika nyingi zaidi
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ameonyesha kuvutiwa na Miquissone ambapo amesema mchezaji huyo ataongeza makali ya safu yake ya ushambuliaji
Simba inachuana na Azam Fc katika mchezo ambao ni wa tatu baina ya timu hizo msimu huu
Simba ilishinda mechi zote mbili zilizopita
ADVERTISE HERE