Simba vs Azam Fc, nusu fainali ya kibabe kombe la Mapinduzi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Jan 2020
Simba vs Azam Fc, nusu fainali ya kibabe kombe la Mapinduzi

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba majira ya saa mbili na robo usiku wa leo watashuka kwenye uwanja wa Amaan kumenyana na Azam Fc katika mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi

Mshindi wa mchezo huo atatinga fainali ambapo katika hatua hiyo atachuana na Mtibwa Sugar iliyoiondosha Yanga kwa mikwaju ya penati jana

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkali hasa ukizingatia ubora wa timu zote

Mwaka jana timu hizo zilikutana fainali na Azam Fc kuibuka mabingwa kwa ushindi wa mabao 2-1

Msimu huu tayari zimekutana mara mbili, mchezo wa Ngao ya Jamii ambao Simba ilishinda 4-2 na kwenye ligi Simba ikiibuka kwa ushindi wa bao 1-0

Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema wanatarajia kupata upinzani mkali kutoka kwa Azam Fc lakini lengo lao ni kutinga fainali ya michuan hiyo ambayo ni maalum kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck anatarajia kutumia kikosi chake cha kwanza kwani nyota wote wa timu hiyo wako visiwani Zanzibar

Mashabiki wa Simba walikuwa na shauku kubwa ya kukutana na Yanga hatua ya fainali, kutolewa kwa Yanga kunaweza kupunguza msisimko hasa ikizingatiwa huenda kusiwe na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’