Tumejiandaa vizuri kuwakabili Azam Fc - Matola

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Jan 2020
Tumejiandaa vizuri kuwakabili Azam Fc - Matola

Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam Fc hautakuwa mwepesi

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake, Matola amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali

Matola amesema Azam Fc ni moja ya timu bora Tanzania kutokana na uwekezaji mkubwa waliofanya

"Mchezo huo hautakuwa mwepesi kwa kuwa tunakwenda kucheza na moja ya timu bora nchini. Wachezaji wetu wako tayari, tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri," amesema Matola

Akizungumzia mabadiliko ya mara kwa mara ya kikosi yanayofanywa na kocha Sven Vandenbroeck, Matola amesema wanalazimika kufanya hivyo kutokana na ratiba ya mechi zinazowakabili

"Tumetoka kucheza mechi za ligi mfululizo, na michuano hii ya Mapinduzi kwa wastani tunacheza kila baada ya siku tatu. Wachezaji wetu sio roboti lazima tuwape muda wa kupumzika. Mara nyingi tumesema katika kikosi chetu, kila mchezaji anaweza kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza"

Simba itamenyana na Azam Fc kesho Ijumaa katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Amaan saa mbili na robo usiku

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’