Bocco anaamini nafasi ya Okwi iko wazi Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Jan 2020
Bocco anaamini nafasi ya Okwi iko wazi Simba

Nahodha wa Simba, John Bocco amesema pengo la Emmanuel Okwi bado linaonekana ndani ya kikosi chao na ndio sababu ya wao kushindwa kufunga mabao mengi.

Msimu uliopita safu ya ushambuliaji ya Simba ilifunga jumla ya mabao 53 huku Bocco akifunga mabao 14, Okwi (16) na Meddie Kagere mabao 23.

Bocco jana aliifunga bao moja Simba ikishinda 3-1 dhidi ya Zimamoto kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi na kufuzu kwa nusu fainali.

Nahodha huyo alisema Okwi bado anahitajika kwenye kikosi chao licha ya Kagere kufanya vizuri, lakini mapungufu yaliyopo kwenye safu ya ushambuliaji yanaonyesha pengo la Mganda huyo.

Bocco alisema Okwi alikuwa haziachi nafasi anazozipata, tofauti na Kagere ambaye akitengenezewa nafasi tano basi yeye atafunga mbili au moja.

“Siyo kama Kagere hafanyi vizuri hapana, Kagere ni mshambuliaji mzuri, lakini tofauti na Okwi ambaye hajawahi kupoteza nafasi hata moja anayotengenezewa amekuwa hafanyi makosa sehemu za hatari tofauti na Kagere,” alisema Bocco.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
30m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’