Mabingwa wa nchi Simba wametinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuwalaza Zimamoto mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Gombani, Pemba
Simba ilifunga mabao mawili ya haraka haraka kwenye dakika ya nne na tisa kupitia kwa nahodha John Bocco na Sharaff Shiboub
Ibrahim Ajib akaongeza bao la tatu wakati bao pekee la kufutia machozi kwa upande wa Zimamoto lilifungwa na Hamad Hilika
Ushindi huo umeipeleka Simba nusu fainali ya michuano hiyo na sasa itacheza na Azam FC
ADVERTISE HERE