Mkufunzi wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kujiamini kulikopitiliza kwa wachezaji wake kulipelekea wakalazimishwa sare ya mabo 2-2 dhidi ya Yanga juzi
Mchezo huo wa ligi kuu, uliishuhudia Simba ikipoteza uongozi wa mabao 2-0 na kulazimishwa sare ya mabao 2-2
Vandenbroeck alisema timu haikucheza vizuri kwenye kipindi cha pili
“Sijafurahishwa hata kidogo na tukio ambalo nimelishuhudia, kufungwa mabao mawili ndani ya dakika saba hili jambo ni baya na linaumiza, wachezaji hawajafanya kile ambacho nilitarajia mwanzo.
“Ninaamini kwamba walishindwa kujituma na kulinda ushindi waliopata kutokana na kujiamini kupita kiasi na kusahau kwamba mpira unaendelea, nitakaa na wachezaji wangu kuzungumza nao kwani hawajafanya vizuri kuruhusu mabao waliyoanza kufunga,” alisema Sven