Simba yaomba sapoti ya mashabiki kombe la Mapinduzi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Jan 2020
Simba yaomba sapoti ya mashabiki kombe la Mapinduzi

Uongozi wa klabu ya Simba umewataka mashabiki wake kusahau matokeo ya mchezo dhidi ya Yanga na kuiunga mkono timu ambayo iko visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi

Juzi Simba ililazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Yanga katika mchezo ambao timu hiyo ilikuwa na kila sababu ya kushinda lakini ikaruhusu mabao mawili ndani ya dakika tano

Ni matokeo ambayo hayakuwafurahisha mashabiki ambao tangu juzi wana majonzi

Bosi wa kitendo cha Habari Simba Haji Manara, amesema mashabiki wanapaswa kusonga mbele kwa kusahau kilichotokea dhidi ya Yanga

Aidha amesema wanapaswa kuiunga mkono timu yao ambayo tayari iko visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi

"Baada ya masaa ishirini na nne ya maumivu makali ya kutoka sare na timu ambayo ishasahau kabisa kutufunga, naamini sasa mihemko yetu Wanasimba itakuwa imeisha au kupungua"

"Hatujafungwa bali tumedroo,tusiendeleze tena lawama ( madukuduku yaishe) turudi mstarini na kuhakikisha tunamaintain status yetu. Twendeni Zanzibar kwa nguvu kubwa na kurudi kutetea ubingwa wetu," amesema manara

Simba itashuka dimba la Gombani kesho kuikabili Zimamoto katika mchezo ambao kama watashinda watatinga hatua ya nusu fainali

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’