Kwa mara nyingine leo mlinda lango Aishi Manula ameingia lawamani baada ya kuruhusu mabao mepesi kwenye mchezo dhidi ya Yanga
Simba ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0 kabla ya Yanga kurudisha mabao hayo ndani ya dakika tatu
Manula amekuwa na udhaifu wa kushindwa kucheza mipira inayopigwa nje ya 18
Bao alilofunga Balama ni aina ya mabao ambao Manula amekuwa akiruhusu sana
Lakini pia mawasiliano mabovu kati yake na Mohammed Hussein yalipelekea Zimbwe kujifunga bao la pili
Mlinda lango namba mbili Beno Kakolanya amekuwa akifanya vizuri kila anapopewa nafasi
Pengine ni wakati wa kumpa nafasi Beno zaidi ili kumjenga Manula aweze kufanyia kazi changamoto zinazomkabili
Kwani amekuwa akiruhusu mabao ya aina moja
Baada ya mchezo leo mashabiki wa Simba wametoa maoni yao kuhusu kiwango cha Manula
Wengi hawakufurahishwa na mabao aliyofungwa leo