Ushindi dhidi ya URA kuipeleka Simba nusu fainali kombe la Mapinduzi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Jan 2018
Ushindi dhidi ya URA kuipeleka Simba nusu fainali kombe la Mapinduzi
Jana Simba ilikubali kipigo kwa mara ya pili mfululizo kutoka kwa Azam FC kwenye kombe la Mapinduzi baada ya kuchapwa 1-0 ikiwa ni mchezo wa Kundi A.

Timu hizo zilikutana kwenye mchezo wa fainali mwaka jana na Azam wakaifunga Simba 1-0.

Azam inaongoza Kundi A kwa kufikisha pointi tisa baada ya kucheza mechi nne, URA ina pointi saba katika nafasi ya pili, Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne huku Mwenge na Jamhuri zenyewe zikiwa hazipo kwenye mbio za kuwania kufuzu hatua ya nusu fainali.

Vita kubwa katika kundi hilo inabaki wa Simba na URA ambazo zote zina nafasi ya kusonga mbele kucheza nusu fainali ya Mapinduzi, timu hizo zitakutana katika mchezo wa mwisho ambao utaamua ni gani inaungana na Azam kutoka Kundi A kwenda kucheza nusu fainali.

Matumaini pekee ya Simba yapo kwenye mchezo wao dhidi ya URA, Simba inahitaji ushindi ili kufuzu kwa wastani wa magoli.

Katika mechi zake mbili, Simba imefunga magoli matatu huku yenyewe ikifungwa mawili hivyo kufanya wastani wa magoli kuwa ni goli moja.

URA inawastani wa magoli mawili kwa hiyo kama Simba itashinda mechi yake dhidi ya URA itaungana na Azam kucheza nusu fainali.

Matokeo ya sare au kufungwa na URA yataifanya Simba kutupwa nje ya mashindano katika hatua ya makundi hivyo watakuwa wameondolewa katika taji jingine ndani ya siku 16 hiyo ni baada ya kutolewa katika kombe la Azam Sports Federation Cup December 22, 2017 kwa kufungwa na Green Warriors kwa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia sare ya kufungana 1-1.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
15h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’