Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kikosi chake kiko tayari kuelekea mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa kesho Jumamosi, uwanja wa Taifa
Akizungumza na wanahabari mapema leo kuelekea mchezo huo, Sven amesema ni wachezaji wawili tu Miraji Athumani na Rashid Juma ambao hawataweza kuwa sehemu ya kikosi kwa ajili ya mchezo huo
"Tumefanya maandalizi ya kutosha, wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo isipokuwa Miraji na Rashid," amesema Sven
Naye nahodha John Bocco amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono
Amesema pamoja na kuiheshimu Yanga lakini wana kikosi bora, nafasi ya kuibuka na ushindi ni kubwa
ADVERTISE HERE