Sven ameshawasoma Yanga, wajiandae 'kisaikolojia'

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Jan 2020
Sven ameshawasoma Yanga, wajiandae 'kisaikolojia'

Mkufunzi wa Simba, Mbelgiji Sven Vanderbroek amesema hana hofu na pambano la watani wao, Yanga litakalopigwa Jumamosi kwa madai tayari ameshaisoma mapema, huku akisisitiza kurejea uwanjani kwa nahodha John Bocco na Erasto Nyoni kwao ni faida kubwa.

Sven aliyeipokea timu kutoka kwa Mbelgiji mwenzake, Patrick Aussems amesema anauchukulia mchezo wao wa Jumamosi kwa uzito mkubwa, lakini anachofurahia ni kupata wasaa wa kuisoma Yanga mapema, hivyo haoni kama watawasumbua kwenye Uwanja wa Taifa.

Kocha huyo aliyeiongoza Simba katika mechi nne, ikiwamo moja ya Kombe la FA na tatu za Ligi Kuu Bara na kushinda zote wakipiga jumla ya mabao 14 bila kufungwa lolote, alisema ushindi mfululizo kwao ni faraja ya kuingia kwenye mchezo wa Jumamosi wakiwa na ari kubwa.

Alisema licha ya kuwa na muda mfupi nchini, lakini amepata wasaa wa kuwasoma Yanga katika mechi zao kadhaa walizocheza ili kujua uimara na udhaifu wao na kilichobaki kwake ni kupata jeshi lake ili waendeleze wimbi lao la ushindi na kuzidi kujikita kileleni.

“Najua haitakuwa mechi rahisi, pambano la wapinzani wa jadi ni kubwa na lazima lichukuliwe kwa uzito mkubwa ila nimefurahia kuimarika kwa kina John Bocco na Erasto Nyoni,” alisema na kuongeza;

“Bado naendelea kuwafuatilia wapinzani tunaokutana nao ili kuzidi kufahamu namna ya kuwakabili tukiwa na ubora zaidi yao. Nafahamu nina wachezaji wengi wenye vipaji na wabunifu kwa kila mbinu ninazowapa wakizifanyia kazi sioni nafasi ya kushindwa kufanya vizuri.”

Alisema wachezaji hao ndio atakaowatumia katika mechi dhidi ya Yanga ili wapate ushindi kwani anaamini ubunifu wanapokuwa na mpira, uwezo wa kujiamini na kutimiza majukumu yao kwa wakati utawabeba Taifa.

“Mechi zote ni kama fainali na huwezi kuweka akili kuwa zipo ndogo hivyo za kupuuza, si kweli lazima uweke nguvu kote, lakini mechi na Yanga ni tofauti kabisa kwa sababu ni timu na mechi tofauti,” alisema Sven.

Akizungumzia kurudi kwa Bocco na Nyoni alisema amefurahi kuwaona uwanjani.

“Nimefurahi kuona namna Bocco na Nyoni walivyoimarika na kucheza dakika 90, kwangu ni jambo zuri. Pia, kitendo cha Kanda (Deo) na Kahata (Frances) kufunga imeniongezea nguvu zaidi kwenye kikosi changu,” alisema Sven.

Sven alifichua michezo minne aliyocheza dhidi ya AFC Arusha na kushinda 6-0, kisha kuzichapa Lipuli (4-0, KMC (2-0 ) na Ndanda (2-0) juzi katika Ligi Kuu zimempa aina ya kikosi anachopaswa kukitumia kuimaliza Yanga.

“Ndani ya mechi hizo, nimepata picha nzuri na kujua ubora na udhaifu wa timu yangu na wachezaji nilionao, bado kuna baadhi yao hawako vizuri katika utimamu wa akili na ustahimili wa mwili kwenye kasi na mengine,” alisema Sven, huku akisisitiza kuna mambo makuu mawili aliyoyafanyia kazi kama mfumo na namna ya uchezaji kwa vijana wake bila kuweka hadharani.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’