Jonesia apewa rungu mechi dhidi ya Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Jan 2020
Jonesia apewa rungu mechi dhidi ya Yanga

Mwamuzi wa kati, Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuchezesha pambano la watani wa jadi, Januari 4, 2020 kati ya Simba dhidi ya Yanga, Uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo mwamuzi Jonesia kutoka Kagera atasaidiwa na msaidizi namba moja, Sudi Lila huku namba mbili akiwa, Hamisi Chang'walu wote wa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa TFF, mwamuzi wa akiba ni Elly Sasii wa Dar es Salaam huku Kamishna wa mchezo huo akiwa Khalid Bitebo wa kutoka Mwanza na Mtathimini waamuzi ni Sudi Abdi ambaye anatokea Arusha.

Kigezo cha kwanza Jonesia ni mwamuzi wa Kimataifa mwenye Beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), pili ni amefanya vizuri kwenye mitihani na mazoezi ya utimamu kupima ubora na ufanisi wa marefa na tatu ameteuliwa kuchezesha fainali za dunia za wanawake na Afcon kwa Vijana 2019.

Jonesia ambaye atachezesha pambano la Simba na Yanga, mwishoni mwa mwaka juzi, alichezesha fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) kwa wanawake zilizofanyika nchini Ghana kuanzia Novemba 17 hadi Desemba mosi.

Mwamuzi Jonesia anaingia kuchezesha mchezo wake wanne wa mechi ya watani huku akiwa na rekodi kutoa kadi nyekundu kwa michezo miwili aliyochezesha awali.

Hivyo wachezaji wa Simba na Yanga watalazimika kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu ili kukwepa kadi nyekundu za mwamuzi Jonesia Rukyaa

Mhanga wa kwanza alikuwa nahodha wa Yanga, Kelvin Yondani ambaye katika mechi ya Mtani Jembe alilimwa kadi nyekundu kwa kumchezea madhambi Ramadhani Singano 'Messi'.

Pia alipochezesha mara ya pili kwenye Ligi Kuu mwaka 2016, aliyekuwa beki Abdi Banda wa Simba alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea madhambi Donald Ngoma.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’