Mtendaji wa Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amebainisha kuwa wamemruhusu mshambuliaji Wilker Da Silva raia wa Brazil kwenda kufanya mazungumzo ya kujiunga na moja ya timu huko Malaysia
Ni wazi Simba imefikia makubaliano na Wilker kumruhusu aondoke kwenda kutafuta maisha mahali pengine
Uamuzi huu haukuwastua wengi, kwani ni maamuzi ambayo mashabiki wa Simba walikuwa wakiyasubiri
Ukiondoa suala la kukaa nje mara kwa mara kutokana na majeraha, Wilker alishindwa kutamba kwenye kikosi cha Simba
Aliifungia Simba bao moja tu kwenye mchezo wa kirafiki
Ni mchezaji ambaye kiwango chake ni cha kawaida, bila shaka, nafasi yake Simba italeta mshambuliaji ambaye atakuwa na mchango mkubwa kwa timu
Katika usajili uliopita Simba ilisajili nyota watatu raia wa Brazil wengine wakiwa Gerson Fraga na Tairone Da Silva
Fraga anafanya vizuri kila anapopewa nafasi kama ilivyo kwa Tairone ingawa bado wachezaji hao wanaonekana kuwa na viwango vya kawaida