Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema kabla ya wiki hii kumalizika, watamtambulisha mchezaji mpya ambaye usajili wake umekamilika
Wakati dirisha dogo la usajili likiwa limefunguliwa, Simba haionekani kuwa busy na usajili kama watani zao Yanga
Pengine ni kutokana na uimara wa kikosi cha mabingwa hao wa nchi hivyo kutokuwa na sababu ya kufanya usajili mkubwa
"Hatukurupuki kusajili kwani uamuzi huo unategemea na mapendekezo ya wadau hasa benchi la ufundi. Wiki hii tunatarajia kumtangaza mchezaji tuliyemsajili, " alisema Senzo
Aidha Senzo amekanusha taarifa ya kutolewa kwa mkopo kinda Rashid Juma kwenda klabu ya Majimaji
Senzo amesema Rashid ni majeruhi na anaendelea na matibabu
ADVERTISE HERE