Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza viingilio vya mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumamosi, Januari 04 kwenye uwanja wa Taifa
Akizungumza na wanahabari mapema leo, Msemaji wa Simba Haji Manara ametaja viingilio hivyo kuwa VIP A ni Tsh 30,000/-, VIP B na C ni Tsh 20,000/- wakati mzunguuko ni Tsh 7,000/-
Manara amewataka mashabiki kuchangamkia tiketi hizo ili kuhakikisha wanaujaza uwanja wa Taifa kutokana na wingi wao dhidi ya watani zao Yanga
Aidha kuelekea mchezo huo, Manara amesema Simba itaingia ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mechi nyingi dhidi ya Yanga katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
"Pamoja na kuwa timu yetu ni bora kuliko yao na tumeshinda mechi nyingi dhidi yao, hatutawadharau," alisema Manara
ADVERTISE HERE