Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wamefunga mwaka kwa ushindi mnono wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa
Ulikuwa ni mchezo wa upande mmoja kwa muda mwingi, Simba ikitawala kwa soka safi la pasi fupifupi
Francis Kahata aliitanguliza Simba kwa bao la mpira wa adhabu kwenye dakika ya 13 kabla Deo Kanda hajaongeza la pili kwenye dakika ya 85

Ushindi huo umeifanya Simba iendelee kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 10 baada ya kufikisha alama 34
Sasa mchezo unaofuata ni dhidi ya Yanga Januari 04, 2020
Bila shaka salamu zimewafikia...!
ADVERTISE HERE