Simba iko uwanja wa Taifa ikimenyana na Ndanda Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Francis Kahata amewatanguliza mabingwa hao wa nchi kwa bao la mapema tu dakika ya 13 kupitia mpira wa adhabu
Kabla ya mchezo huo, kocha mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck alitaja sababu ya kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake kwenye michezo ya hivi karibuni
Sven amesema anataka kuona uwezo wa kila mchezaji ambaye yuko kwenye kikosi cha Simba
“Lengo la kufanya ‘Rotation’ kwenye kikosi ni kuona kila mchezaji akipata nafasi kwa ajili ya kutathmini viwango vyao. Kwa maana uwezo unaoweza kuona mazoezini ni tofauti na kwenye mechi,” alisema
"Pia nafanya ‘Rotation’ ili kuwapa mapumziko baadhi ya wachezaji kutokana na kucheza mechi mfululizo ndani ya siku chache"
Kwenye mchezo wa leo dhidi ya Ndanda Fc, Sven amefanya 'rotation' kama ulivyokuwa mchezo dhidi ya KMC