Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba, jioni ya leo kitashuka katika uwanja wa Taifa kumenyana na Ndanda Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Huo utakuwa mchezo wa mwisho kwa mwaka 2019, matokeo yake yataingia katika vitabu vya kumbukumbu
Lakini pia, ni mchezo ambao Simba inarejea uwanja wa Taifa, dimba ambalo msimu uliopita lililkuwa machinjio ya vigogo wa soka barani Afrika kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Ni hapohapo mchezo dhidi ya Yanga utapigwa siku ya Jumamosi
Kwa kasi ambayo Simba wanayo, ni mchezo ambao Ndanda Fc wana kila sababu ya kuingiwa na hofu kwani kama hawatakuwa makini wanaweza kuondoka na kapu la mabao
Ndanda Fc wanashika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama nane tu baada ya kushuka dimbani mara 13
Ushindi kwa Simba utawakita kileleni kwa tofauti ya alama 10 dhidi ya wapinzani wao Yanga ambao wanashika nafasi ya pili