Pamoja na ushirikiano mzuri uliopo kati ya viongozi na wachezaji wa Simba, kiungo Gerson Fraga amesema mashabiki wa Simba wanachangia timu hiyo kuendelea kufanya vizuri kwenye ligi
Fraga amesema mashabiki wa timu hiyo wanawapa hamasa wachezaji na kuwafanya wajitume zaidi ili kuhakikisha wanawapa furaha
Fraga ni mmoja wa wachezaji watatu raia wa Brazil ambao walitua Simba mwanzoni mwa msimu
Aidha kiungo huyo kiraka amesema anajivunia kucheza soka Tanzania, ni nchi yenye amani na utulivu
"Ushirikiano kati na wachezaji na viongozi bila ya kuwasahau mashabiki wetu ni sababu ya sisi kuendelea kufanya vizuri," amesema Fraga
"Lakini pia nafurahi kucheza Tanzania kwani ni nchi yenye Amani na Utulivu"
Fraga ameifungia Simba mabao mawili, moja akifunga kwenye ligi na jingine michuano ya kombe la FA