Winga wa Simba Rashid Juma amepelekwa kwa mkopo klabu ya Majimaji Fc inayoshiriki ligi daraja la kwanza
Majimaji imethibitisha kumnasa kinda huyo aliyekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Simba
Rashid ameanza mazoezi hivi karibuni baada ya kuwa nje kwa wiki kadhaa akisumbuliwa na majeruhi
Hii sio mara ya kwanza kwa klabu ya Majimaji kusajili mchezaji wa Simba kwa mkopo
Marcel Kaheza alitolewa kwa mkopo kwenye klabu hiyo mwaka 2017 kisha kurejeshwa Simba msimu uliofuata baada ya kufanya vizuri
Msimu huu ametolewa tena kwa mkopo kwenda klabu ya Polisi Tanzania
ADVERTISE HERE