Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC jana, kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kitashuka dimbani keshokutwa Jumanne, Disemba 31 kufunga mwaka kwa kuwakaribisha Ndanda Fc
Mabingwa hao wa nchi watakuwa na nafasi ya kuendelea kuchanja mbuga kuelekea ubingwa wa tatu mfululizo kama watashinda mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Uhuru
Kocha Sven Vandenbroeck na Kocha Msaidizi Selemani Matola watataka kuendeleza moto ya kugawa vipigo kwa kila anayekuja mbele yao
Chini yao Simba imeimarika zaidi ikifunga mabao 12 katika michezo mitatu iliyopita ambao ni wastani wa mabao manne kwenye kila mchezo
Pengine ni mchezo ambao idadi kubwa ya mabao itaweza kushuhudiwa pia
Baada ya mchezo huo, mabingwa hao watetezi watafungua mwaka 2020 kwa kuwakabili watani zao Yanga katika mchezo ambao utapigwa Januari 04 kwenye uwanja wa Taifa