Vandenbroeck ataja siri ya ushindi dhidi ya KMC

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Dec 2019
Vandenbroeck ataja siri ya ushindi dhidi ya KMC

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya KMC jana ni matokeo ya wachezaji wake kujituma pamoja na kutekeleza maelekezo wallyopewa wakati wa mapumziko

Kwenye mchezo huo uliopigwa uwanja wa Uhuru, Simba ilifunga mabao yake yote mawili kwenye kipindi cha pili kupitia kwa Deo Kanda na Gerson Fraga

"Kipindi cha kwanza hatukucheza vizuri lakini kila mmoja ameona jinsi tulivyorejea tukiwa bora katika kipindi cha pili," Vandenbroeck aliwaambia waandishi wa habari baada ya mchezo huo

"Wakati wa mapumziko tuliwaelekeza wachezaji kuwa tulihitaji zaidi ya kile walichofanya kwenye kipindi cha kwanza, tulihitaji kutengeneza nafasi na muhimu zaidi ni kuzitumia"

"Kwangu mimi mlinda lango wa KMC (Nihimana) alikuwa nyota wa mchezo kwani kama sio umahiri wake tungeweza kushinda kwa mabao mengi zaidi"

Vandenbroeck ameeleza kushangazwa na nafasi wanayoshika KMC, kwani ni timu nzuri

"Nashangazwa na alama ambazo timu hii imekusanya, wanaonekana ni timu nzuri, nadhani walistahili kuwa katika nafasi zuri zaidi kwenye msimamo"

Ushindi huo uliendelea kuikita Simba kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 31, alama saba zaidi ya Kagera Sugar inayoshika nafasi ya pili

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’