Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo wameendelea kugawa dozi kwa timu pinzani ligi kuu ya Vodacom baada ya kuilaza KMC mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck leo alifanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha kwanza ambapo aliwapa nafasi wachezaji ambao huwa hawaanzi mara kwa mara
Kwenye kipindi cha kwanza, pamoja na changamoto ya uwanja wa Uhuru kuathiriwa na mvua zinazonyesha jijini Dar es salaam, Simba haikuonekana kuwa kwenye ubora wake
Hata hivyo vijana wa Sven walirejea kipindi cha pili wakiwa imara na alikuwa ni Deo Kanda aliyefunga bao la kwanza muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha pili

Kiungo Gersona Fraga nae akafunga bao la pili kwenye dakika za majeruhi na kuihakikishia Simba alama tatu muhimu
Huo ni ushindi wa tatu mfululizo kwa Sven ambaye mpaka sasa timu haijaruhusu bao chini yake
Simba imezidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 31
Inaongoza kwa tofauti ya alama saba dhidi ya Kagera Sugar inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 24