Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo kinarejea uwanja wa Uhuru wakiwa wageni wa KMC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Vinara hao wa ligi watakuwa na nafasi ya kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo
Simba inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama 28, alama nne zaidi ya Kagera Sugar inayoshika nafasi ya pili
Chini ya kocha Sven Vandenbroeck Simba imekuwa ya moto zaidi, ikifunga mabao 10 katika michezo miwili iliyopita bila ya kuruhusu bao
Ni mwenendo huo ambao unawapa kila sababu ya kutamba mashabiki wa mabingwa hao wa nchi
Pengine leo kutashuhudiwa kalamu nyingine ya mabao dhidi ya KMC inayoshika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kuanza saa kumi kamili jioni
ADVERTISE HERE