Dabi ya Simba na Yanga ni kama Ulaya - Sven

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Dec 2019
Dabi ya Simba na Yanga ni kama Ulaya - Sven

Mkufunzi wa klabu ya Simba Sven Vandenbroeck amesema hamasa ya mchezo wa watani wa jadi nchini anaweza kufananisha na mechi kubwa za wapinzani barani Ulaya zinazohusisha timu za Italia (AC Milan na Inter Milan) na hata Hispania (Real Madrid na Fc Barcelona)

Sven aliyetua Simba mapema mwezi huu kuchukua nafasi ya Patrick Aussems aliyetimuliwa, alipata nafasi ya kufuatilia mchezo kati ya Simba na Yanga wakati akiwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zambia

"Wakati nikiwa kocha wa Zambia nilifahamu ukubwa wa mchezo huu, nilikuwa nikimfuatilia Chama (Clatous) ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji katika kikosi changu," alisema

"Ukubwa wa mchezo huu hauna tofauti na mechi nyingine kubwa za wapinzani barani Ulaya. Hapa mashabiki wanazipenda sana timu zao, ni mchezo ambao matokeo yake huamsha furaha upande mmoja na kusababisha majonzi makubwa upande mwingine"

"Ni aina ya mchezo ambao kila mchezaji ana ndoto ya kushiriki"

Simba inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa Januari 04 2020 katika uwanja wa Taifa

Huo utakuwa mchezo wa kufungua mwaka 2020 lakini pia utakuwa mchezo wa kwanza wa dabi kwa Sven ambaye ameanza vyema majukumu yake kunako klabu ya Simba

Chini yake Simba imeshinda mechi zote mbili walizocheza huku wakifunga mabao 10 bila ya kuruhusu bao hata moja

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’