Rage aitabiria Simba ushindi wa mabao saba dhidi ya Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Dec 2019
Rage aitabiria Simba ushindi wa mabao saba dhidi ya Yanga

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage amesema kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania Bara kiko imara na hakitishwi na mbwembwe za usajili zinazofanywa na Yanga

Akizungumza kuelekea mchezo baina ya timu hizo ambao utapigwa Januari 04 2020, Rage amesema itakuwa vyema kama TFF itawaruhusu Yanga wawatumie wachezaji wao wote waliowasajili dirisha dogo ili wasiwe na visingizio

Amesema kwa uimara wa Simba, pengine itawachukua Yanga karne moja kuweza kupata ushindi dhidi ya mabingwa hao wa nchi

"Mimi nawaonea Yanga huruma, labda nichukue wito huu kuwaomba TFF kama kuna wachezaji wa Yanga ambao usajili wao haujakamilika, sisi hatutaki wapate kisingizio. Namuomba Rais Karia na Kamati zake wawaruhusu hao wachezaji wao wote," alitamba Rage

"Simba imekuwa imara zaidi wakati huu wa kocha mpya pengine kuliko hata enzi za Aussems"

"Aussems alikuwa mzuri katika mchezo wa pasi na kumiliki mpira lakini huyu mpya amekuja na mbinu za kufunga mabao ndio maana mechi zake mbili tu Simba imefunga mabao 10"

"Wakipata bahati siku ya tarehe nne, kama hatukuwafunga saba, sijui itakuwaje. Nawaomba sana wapenzi wa Yanga ambao wana matatizo ya kiafya kama presha wasije uwanjani siku hiyo"

Zimebaki takribani siku nane kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
12h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’