Kiungo mshambuliaji wa Simba Hassan Dilunga jana alifunga mabao mawili na kuwasaidia mabingwa hao wa Tanzania Bara kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Lipuli Fc
Akizungumza baada ya mchezo huo Dilunga alisema ushindi waliopata ni mafanikio ya utekelezaji wa mpango wa mchezo waliopewa na kocha Sven Vandenbroeck
"Ubora wetu leo ni kutokana na kuzingatia mafunzo tuliyopewa na Mwalimu. Kwa kiasi kikubwa tumezingatia kile ambacho tumefundishwa mazoezini," alisema
"Tulihitaji kushinda mchezo huu na lengo ni kushinda kila mchezo unaokuja mbele yetu ili tuweze kutetea ubingwa wetu tuliotwa mwaka jana"
Pengine Dilunga angeweza kuondoka na hat-trik jana kama angetumia nafasi nyingine alizopata katika mchezo huo ambao Simba waliwazidi wapinzani wao kwa kiasi kikubwa