Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo wameifanya sikukuu ya Krismasi kuwa ya furaha zaidi kwa mashabiki wake baada ya kuifumua Lipuli Fc mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Uhuru
Vinara hao wa ligi kuu wameendeleza mwendo wa vipigo leo wakifunga mabao yao kupitia Francis Kahata, Meddie Kagere na Hassan DIlunga aliyekuwa 'moto' leo akifanikiwa kupachika mabao mawili moja akifunga kupitia mkwaju wa penati

Furaha ya mashabiki ilinogeshwa na burudani ya kandanda safi kutoka kwa mabingwa hao wa nchi ambao wamezidi kujichimbia kileleni baada ya kufikisha alama 28
Aidha kinara wa mabao Kagere amerejea katika kiwango chake cha kuzifumania nyavu akifunga katika mchezo wa pili mfululizo
Kagere amefikisha mabao 9
Simba imepachika mabao 10 katika michezo miwili iliyopita, huu ni mwanzo mzuri sana kwa kocha Sven Vandenbroeck