Simba v Azam FC kukumbushia fainali ya mwaka jana

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Jan 2018
Simba v Azam FC kukumbushia fainali ya mwaka jana
Timu za Simba na Azam baadae zitakumbushia fainali ya Kombe la Mapinduzi ya mwaka 2017, wakati zitakapokutana katika hatua ya makundi.

Azam FC na Simba zitachuana katika mchezo wa kundi A, michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea kwenye Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.

Mchezo huo ambao umepangwa kuanza majira ya 2:15, unakumbushia fainali ya mwaka jana ya michuano hiyo ambapo Azam FC, iliibuka na ushindi wa bao 1-0, na kutwaa taji hilo kwa mara ya pili tangu kuanza kushiriki michuano hiyo ya Mapinduzi.

Timu hizo zinakuta zikiwa katika hali tofauti Azam ambao huo ni mchezo wa mwisho wanahitaji kushinda ili wafuzu hatua ya nusu fainali wakati Simba nayo inalazimika kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua hiyo ikikabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa URA inayoongoza ikiwa na alama saba.

Mchezo dhidi ya Azam FC unatarajiwa kuwa mtihani wa kwanza mgumu kwa kikosi cha Simba, ambacho kwa sasa kinanolewa na kocha Masoud Djuma, ambaye tangu amekabidhiwa majukumu ya kuwa kaimu kocha mkuu amebadilisha mfumo wa uchezaji wa timu hiyo kwa kutumia 3-5-2 ambao umeweza kumsaidia kupata ushindi mnono wa
mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Pemba juzi.

Katika mchezo wa ligi timu hizo zipokutana uwanja wa Azam Complex Dar es Salaam, hazikufungana na kuacha deni kubwa kwa makocha wote wawili ambao hajapata matokeo dhidi ya mwenzake.

Azam ambao ndiyo wenyeji wa mchezo huo, watakuwa na kikosi chao kamili na wanatarajia kufanya mashambulizi
mengi kupitia pembeni huku wakimtegemea zaidi mshambuliaji wake Bernald Arthur katika umaliziaji.

Winga Joseph Mahundi na nahodha Himid Mao, watakuwa na kazi moja ya kumtia majaribuni kipa Emmanuel Mseja ambaye kwa sasa ndiyo amepewa jukumu la kuidakia Simba kwenye michuano hii baada ya Aishi Manula kubaki jijini Dar es salaam akitarajiwa kufunga ndoa leo.

Simba kama walivyoingia kwenye mchezo dhidi ya Jamhuri juzi, wanajua umuhimu wa ushindi katika mchezo huo ambao ndiyo utawapa tiketi ya kuendelea kubaki kwenye michuano hiyo.

Kocha Masoud Djuma, niwazi atalazimika kuongeza idadi ya viuongo kwenye kikosi chake ili kuwadhibiti Azam FC, kwenye eneo la kati kati ya uwanja na kumpa kazi nyepesi mshambuliaji wake John Bocco kuidhuru timu yake ya zamani.

Bila shaka Djuma atamwanzisha Bocco, kwasababu ndiyo mshambuliaji aliyeonyesha kuwa na imani naye sambamba na chipukizi Moses Kitandu ambaye naye ameonekana kuwa na mwendelezo mzuri katika umaliziaji.

Vita kali katika mchezo huo litakuwa kwenye eneo la kiungo ambapo Stephen Kingue,Mao, Joseph Mahundi na Enock Agyei watakuwa na kazi ya kuwadhibiti viungo wa Simba Mwinyi Kazimoto, Mzamiru Yasini, Shiza Kichuya na James Kotei wasiweze kupeleka madhara langoni mwao.

Lakini pamoja na yote walinzi wa Azam wanapaswa kumchunga beki Asante Kwasi kutokana na ujanja wake wa kupanda kusaidia mashambulizi na kufunga kama ilivyotokea kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Jamhuri.

Kulingana na ubora wa timu zote mbili mchezo huo unatarajiwa kuwa wakuvutia na hesabu zaidi na mashabiki wa soka wanausubiria kwa hamu ili kujionea kile kinachokwenda kutokea kwenye uwanja wa Amaan.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’