Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ameanza vyema majukumu ya kuwanoa mabingwa hao nchi baada ya kupata ushindi wake wa kwanza mchezo wa kombe la FA juzi dhidi ya AFC
Pamoja na AFC kuonekana kutokuwa kipimo sahihi kwa Simba, lakini kuna mambo ambao yanaonyesha kufanyiwa kazi na Sven katika muda mfupi aliokaa na timu
Kwanza timu imeendeleza utamaduni wake wa umiliki wa mpira kama ilivyokuwa wakati wa Patrick Aussems
Bado Simba imeendelea kuwa timu bora linapokuja suala la umiliki wa mchezo
Lakini zaidi kunaonekana kuwa na mabadiliko wakati timu inapokwenda kushambulia
Timu inakuwa na idadi ya kutosha ya wachezaji pale inaposhambulia
Pengine ule utegemezi wa mshambuliaji mmoja huenda usiwepo
Ukiangalia mabao sita yaliyofungwa katika mchezo dhidi ya AFC, yaliwekwa kambani na wachezaji sita tofauti
Miongoni mwa waliofunga ni kiungo mkabaji Gerson Fraga ambaye wakati wa Aussems ilikuwa nadra sana kumuona akiwa ndani ya eneo la sita la timu pinzani kama sio mpira ya kona au adhabu
Sasa wachezaji wanaonekana kujituma zaidi na pale mpira unapopotea wanajaribu kuurejesha katika himaya yao kwa haraka
Ingawa bado ni mapema lakini Sven anaonekana kuendeleza pale aliposihia Aussems na bila shaka chini yake Simba itakuwa bora zaidi