Michuano ya kombe la Mapinduzi itaanza mapema mwezi Januari 2020 baada ya mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utapigwa Januari 04 2020
Simba iliyopangwa kundi B pamoja na timu za Mtibwa, Chipukizi na Zimamoto, itashuka dimbani Januari 07 kuumana na Zimamoto
Tofauti na miaka iliyopita, michuano ya msimu huu itafanyika kwa mtoano
Ushindi kwenye mchezo huo utawahakikishia mabingwa hao wa nchi kutinga nusu fainali ambapo katika hatua hiyo watachuana na mshindi wa mchezo kati ya Azam Fc dhidi ya Mlandege
Mchezo wa fainali utapigwa Januari 13 2020
ADVERTISE HERE