Okello, nyota wengine wanaohusishwa na Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Dec 2019
Okello, nyota wengine wanaohusishwa na Simba

Allan Okello amekuwa mchezaji gumzo katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa sasa kutokana na umahiri anaoonyesha timu ya Taifa ya Uganda na klabu anayochezea ya KCCA

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 anawaniwa na klabu kadhaa ambapo kwa hapa Tanzania klabu ya Azam Fc ilikuwa ya kwanza kujitosa kumuwania kabla ya mabingwa wa nchi Simba nao kudaiwa kujiunga

Klabu ya KCCA imeweka bayana kuwa iko tayari kumuuza kiungo huyo fundi lakini dau la usajili lisipungue dola 400,000 ambazo ni zaidi ya Milioni 900 za Kitanzania

Mapema mwezi Juni, Okello alikwenda Uswissi kufanya majaribio kunako klabu ya FC Zurich inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo

Simba inatarajiwa kutumia dirisha dogo la usajili kuboresha kikosi chake, sio ajabu kuhusishwa na mchezaji huyo mahiri

Baadhi ya wachezaji wengine ambao wanahusishwa kuwaniwa na mabingwa hao wa nchi ni pamoja na kiungo Baraka Majogoro anayeitumikia Polisi Tanzania na beki wa timu ya Taifa Bakari Nondo Mwamnyeto anayecheza klabu ya Coastal Union

Wengine ni Shiza Kichuya na Tuisila Kisinda ambao inaelezwa yalikuwa ni mapendekezo ya kocha aliyeondoka, Patrick Aussems

Lakini pia yumo winga Luis Miquissone aliyekuja nchini na UD Songo kucheza na Simba mchezo wa ligi ya mabingwa

Miquissone ndiye aliyeifungia bao lililoivusha UD Songo raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa

Nyota huyo aliitumikia UD Songo kwa mkopo akitokea klabu ya Mamelodi Sundowns

Hata hivyo inaelezwa yuko mbioni kuvunja mkataba wake na Mamelodi

Inaelezwa Mtendaji wa Simba Senzo Mazingisa amesafiri kwenda Afrika Kusini kukamilisha usajili wa nyota huyo ambaye kuna tetesi kuwa anawaniwa na Yanga pia

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’