Simba iko tayari kwa ratiba ya funga mwaka

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Dec 2019
Simba iko tayari kwa ratiba ya funga mwaka

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na Kombe la Shirikisho la Soka nchini maarufu FA Cup dhidi ya Arusha Fc pamoja na michezo ya Ligi Kuu

Kutokana na mabadiliko ya ratiba ya Ligi Kuu Bara yaliyofanywa na Bodi ya Ligi hivi karibuni, Simba itacheza mechi nne Uwanja wa Uhuru kabla ya Januari 4, mwakani kuvaana na Yanga katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuikaribisha Arusha Fc keshokutwa kwenye mechi ya Kombe la FA, Desemba 25 itavaana na Lipuli FC huku siku tatu baadaye ikiwa na kibarua kigumu dhidi ya KMC FC kabla ya kufunga mwaka kwa kuikaribisha Ndanda FC hapo Desemba 31, mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola alisema wachezaji wa kikosi hicho wapo vizuri wakati huu wakiendelea na mazoezi na kufafanua kuwa kila kitu kinakwenda sawa.

"Tunaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya Kombe la Shirikisho pamoja na mashindano ya Ligi Kuu," alisema Matola ambaye ataanza kukiongoza kikosi hicho kwa mara ya kwanza msimu huu akiwa na Kocha Mkuu, Mbelgiji Sven Vandenbroeck baada ya Patrick Aussems kutimuliwa.

Naye msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara akizungumzia usajili wa dirisha dogo, alisema kwa upande wao hawana pupa na kudai watasajili kwa matakwa ya kocha wao ambaye anaendelea kukisoma kikosi hicho baada ya kukikabidhiwa hivi karibuni.

Alisema endapo kocha atahitaji kuongeza au kupunguza mchezaji yeyote, watasajili na kudai wapo imara idara zote kwa sasa.

"Sisi hatuna pupa ya usajili tutasajili kwa matakwa ya kocha wetu hatusajili kwa ajili ya kufurahisha watu," alisema Manara.

Aliendelea kusema wanaendelea kujipanga kwa ajili ya kukutana na mahasimu wao Yanga, Januari 4 Mwakani.

"Yanga wanasajili kila siku, lakini tukutane Januari 4 Taifa," alisema.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
4h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
10h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’